LATEST POST

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani ‘PASCAL KABOMBE

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani 'PASCAL KABOMBE. "Kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu usajili wa dirisha dogo kwa timu mbalimbali japo kwa...

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba. “Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya...

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland, Antoine Griezmann

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland na Antoine Griezmann wote waliongeza idadi yao katika mechi zao za...

Nusu Finali ni ya Al Ahly Vs Esperance Sportive de Tunis na Mamelodi Sundowns Vs TP Mazembe

Nusu Finali ni ya Al Ahly Vs Esperance Sportive de Tunis na Mamelodi Sundowns Vs TP Mazembe. Vilabu mashuhuri barani Afrika, Al Ahly ya...

Usiku wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa CAFCL April 5, 2024

Michezo michezo miwili ya Ligi Ya Mabingwa Barani Afrika CAFCL ulipigwa usiku wa Ijumaa kati ya miamba wa Miisri Al Ahly dhidi ya Simba...

KIMENUKA BRUNO GOMES ATIMUKA SINGIDA FOUNTAIN GATE SABABU ZOTE ZAELEZWA

Bruno Gomes Atimuka Singida Fountain Gate. Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Mbrazili Bruno Gomes ametangaza kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande...
SportsYANGA WANAWEZA KUPANGWA KUKIPIGA NA HAWA ROBO FAINAL YA CAF

YANGA WANAWEZA KUPANGWA KUKIPIGA NA HAWA ROBO FAINAL YA CAF

Yanga wanaweza Kupangwa kikipiga na hawa Robo Fainal ya CAF. Baada ya Yanga kumaliza sehemu ya kwanza ya misheni iliyokuwa nayo ya kuvuka hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, japo ilimaliza kwa kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya watetezi wa taji na vinara wa Kundi D, Al Ahly mashabiki wa timu hiyo leo watakuwa wakisikilizia mechi za makundi mengine ili kujua zipi za kukutana nazo.

Kocha Miguel Gamondi aliiongoza kwa mara ya kwanza Yanga ugenini dhidi ya Al Ahly na kupoteza kwa bao 1-0, lakini tayari alishakuwa na tiketi ya robo fainali kutoka kundi hilo baada ya wiki iliyopita kuifyatua CR Belouizdad ya Algeria kwa mabao 4-0 na kuifanya imalize nafasi ya pili licha ya kulingana pointi nane na wapinzani wao hao.

CR Beloiuzdad jana usiku ilipata ushindi wa mabao 3-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana, lakini haikuisaidia kitu mbele ya Yanga kwa vile matokeo ya jumla baina yao, imezidiwa kwani Waalgeria ambao walishinda nyumbani dhidi ya Yanga kwa mabao 3-0, lakini kipigo cha 4-0 Kwa Mkapa kikawatupa nje ya michuano.

Wananchi kwa sasa wanasikilizia matokeo ya mechi zitakazopigwa kuanzia leo saa 10 jioni za makundi ya A, B na C ili kujua itakutana na timu ipi baada ya droo ya mechi za robo fainali itakapofanyika wiki ijayo jijini Cairo.

Yanga inajua haiwezi kukutana na watani wao wa jadi Simba hata kama leo Wekundi wa Msimbazi wataifumua Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa mabao mengi, kwa vile nayo itamaliza kwenye nafasi ya pili katika Kundi B baada ya Asec kujimilikisha nafasi ya kwanza mapema kwa kukusanya pointi 11 katika mechi tano ilizocheza hadi sasa.

Pia Yanga haiwezi kukutana na vinara wa kundi D ilililokuwapo, yaani Al Ahly, lakini klabu nyingine tano ikiwamo Asec Mimosas zenye nafasi ya kumaliza kama vinara wa makundi hayo matatu yanawapa presha kwa sasa Wanayanga.

Kabla ya mechi hizo zitakazopigwa kati ya saa 1:00 usiku na saa 4:00 usiku hesabu zinaonyesha jumla ya timu sita zilikuwa tayari zimeshatinga robo fainali, ila hazijui zitamaliza kwenye nafasi zipi na hivyo kuwafanya Yanga kujua mapema kama haitapangwa na Mamelodi Sundowns kutoka KUndi A, basi lazima iwe ni TP Mazembe iliyokuwa nao kundi moja msimu uliopita katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kuitia aibu hadi timu ya Wananchi ikafika fainali.

Iwapo itatokea ikakosa vigogo hivyo vya Kundi A, basi itaweza kuvaana na Asec ambayo haijawahi kukutana nayo tangu zilipovaana katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 1998 na mechi zote Yanga ikipoteza na kama droo itakuwa upande wao, basi ijiandae kukutana ama Petro Atletico ya Angola au Esperance ya Tunisia kama sio Al Hilal.

Petro kwa sasa ndio inayoongoza Kundi C na kutangulia robo, lakini haina uhakika wa kumaliza kama kinara kwa vile Esperance inayovaana na Al Hilal ina pointi nane, ikiwa ni moja pungufu na waliyonayo Waangola hao, ila kama Wasudan wenye pointi tano wataizima Esperance, yenyewe itamaliza nafasi ya pili na kuiacha Petro ikijimwambafai kileleni, bila kujali matokeo ya mchezo wao dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

SIO KINYONGE

Yanga haijatinga kinyonge katika hatua hiyo na ndio maana ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi ya kufika mbali kwenye michuano hiyo hasa kutokana na kiwango ambacho ilikionyesha kwenye mchezo dhidi ya CR Belouizdad na hata walipokawa wakipigania heshima yao dhidi ya Al Ahly.

Makocha wa zamani wa timu hiyo, Hans van der Pluijm na George Lwandamina ‘Chicken’ wamewapongeza huku wakiwataka kukaza buti katika hatua ya robo fainali kulingana na aina ya timu ambazo wanaweza kukumbana nazo.

Pluijm amesema, hii ni hatua ambayo huwezi kukwepa kukutana na timu bora zaidi lakini Yanga ilionja ladha ya robo fainali tangu ikiwa hatua ya makundi, wanatakiwa tu kufanyia kazi udhaifu ambao ulijitokeza ili kuwa bora zaidi lakini kwa upande wa ubora kama timu wanao mkubwa tu wa kushindana.”

Kwa upande wake, Lwandamina amesema, “Hii ni hatua kubwa ambayo huhitaji kuwa bora maana kosa moja au mawili yanaweza kukugharimu.”

YANGA WANAWEZA KUPANGWA KUKIPIGA NA HAWA ROBO FAINAL YA CAF

YANGA WANAWEZA KUPANGWA KUKIPIGA NA HAWA ROBO FAINAL YA CAF

MAZEMBE/ MAMELODI

TP Mazembe na Mamelodi zote zimefuzu robo fainali kutoka kundi A, lakini bado haijafamika nani kati yao atamaliza katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi hilo wote wamekusanya pointi 10, hivyo mchezo leo wa mwisho unaochezwa Afrika Kusini utaamua kesi yao.

Mmoja kati yao anaweza kukutana na Yanga itategemea na matokeo ya mchezo huo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe, Pretoria.

Mazembe inayopambana kurejea kwenye ubora, msimu uliopita katika Kombe la Shirikisho Afrika ilikiona cha moto kutoka kwa Yanga, kwani ilipigwa nje ndani ikianza kulala 3-1 ugenini kabla ya kulala 1-0 nyumbani kwenye hatua ya makundi.

Pamoja na hayo, Mazembe ni kati ya timu zenye mafanikio kwenye mpira wa Afrika, imetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara tano katika miaka ya 1967, 1968, 2009, 2010, 2015, hivyo inaijua vilivyo michuano hiyo.

Kwa upande wa Mamelodi ipo kwenye kiwango bora ikitoka kuchukua ubingwa wa michuano mipya ya African Football League ‘AFL’ ikibebzwa zaidi na nguvu ya kiuchumi inayowapa jeuri ya kusajili wachezaji kutoka Amerika Kusini na kwingineko kwa mabilioni ya pesa.

Wamekuwa wakifika hatua kama hii mara kwa mara, ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa msimu huu. Nyota 10 wa Mamelodi waliunda kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ kilichofanya makubwa kikifika nusu fainali kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zilizomalizika mwezi uliopita huko Ivory Coast.

ASEC MIMOSAS

Kama Yanga itapewa ASEC Mimosas basi itakuwa ni nafasi kwa Stephane Aziz Ki, Kouassi Attohoula Yao na Pacome Zouzoua kurejea Ivory Coast kucheza dhidi ya waajiri wao hao wa zamani, inaweza kuwa mechi nzuri na ya kuvutia kulingana na uhusiano wa timu hizo mbili.

ASEC ni mkubwa kwa Yanga kama ilivyo kwa Mazembe, Mamelodi, Petro de Luanda na Esperance de Tunis kulingana na viwango vyao kwa nyakati tofauti kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Historia inaonyesha Yanga iliwahi kukutana mara mbili na Asec Mimosas mwaka 1998, zikiwa kundi B na Waivory Coast hao walivuna pointi sita dhidi ya Wananchi walioburuza mkia kwa kuvuna pointi mbili, huku wababe hao wakimaliza vinara kwa pointi 13 mbele ya Manning Rangers na Raja Casablanca.

Kwa sasa Yanga inaonekana kuwa na nguvu kubwa zaidi kiuchumi na ndio maana iliweza kuwanasa wachezaji kadhaa muhimu kutoka kwenye kikosi hicho.

PETRO DE LUANDA/ ESPERANCE

Kesi ya Petro de Luanda na Esperance de Tunis kwenye kundi C ni tofauti kidogo na ile ya TP Mazembe na Mamelodi Sundowns.

Unajua kwanini? Mwenye uhakika wa kusonga mbele ni Petro de Luanda yenye pointi tisa na inamalizana leo na Etoile du Sahel, ila Esperance de Tunis mwenye pointi nane itategemea na matokeo ya mchezo wake wa mwisho pamoja na kwamba anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele maana mchezo wake mwisho yupo nyumbani dhidi ya Al Hilal mwenye pointi tano.

Kwa kiasi kikubwa michezo ya mwisho kwenye kundi hili C ina nafasi kubwa ya kuamua kama ni Petro de Luanda au Esperance de Tunis ambaye atacheza na Yanga au tunaweza kuona maajabu kwa Al Hilal ya Sudan kupindua meza, ni suala la muda, ingawa haitakuwa na nafasi ya kukutana tena na Yanga kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Msimu uliopita Al Hilal iliilazimisha sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya raundi ya kwanza, kisha kushinda nyumbani kwa bao 1-0 na kuifanya Yanga iende kucheza play-off kuwania kucheza makundi Kombe la Shirikisho Afrika na kufanikiwa kwa kuing’oa Club Africain ya Tunisia kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0.

Msimu wa 2007, Yanga ilikutana na Petro de Luanda na Esperance de Tunis katika raundi mbili tofauti wakati akipigania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo kama atapangwa na mmoja kati yao basi wanahistoria ya kukutana nyuma yao.

Yanga ilianza harakati msimu huo katika raundi ya awali ambapo waliing’oa AJSM ya Comoro kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-1 ndipo walipotinga raundi ya kwanza na kukutana na Petro de Luanda, Wananchi walishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0 walipoenda ugenini wakapoteza kwa mabao 2-0 na kusonga mbele.

Safari yao iliishia kwenye raundi ya pili ilikokutana na Esperance kwani kwenye mchezo wa kwanza ilitandikwa kwa mabao 3-0 ziliporejeana jijini Dar es Salaam zilitoka suluhu.

RELATED

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani ‘PASCAL KABOMBE

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani 'PASCAL KABOMBE. "Kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu usajili wa dirisha dogo kwa timu mbalimbali japo kwa...

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba. “Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya...

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland, Antoine Griezmann

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland na Antoine Griezmann wote waliongeza idadi yao katika mechi zao za...