LATEST POST

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani ‘PASCAL KABOMBE

Fred Koublan Sio Mbovu kama wengi anavodhani 'PASCAL KABOMBE. "Kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu usajili wa dirisha dogo kwa timu mbalimbali japo kwa...

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba

Yusuph Manji : Hans Poppe Aivuruga Simba. “Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya...

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland, Antoine Griezmann

Wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa 2023/24: Harry Kane, Kylian Mbappé, Erling Haaland na Antoine Griezmann wote waliongeza idadi yao katika mechi zao za...

Nusu Finali ni ya Al Ahly Vs Esperance Sportive de Tunis na Mamelodi Sundowns Vs TP Mazembe

Nusu Finali ni ya Al Ahly Vs Esperance Sportive de Tunis na Mamelodi Sundowns Vs TP Mazembe. Vilabu mashuhuri barani Afrika, Al Ahly ya...

Usiku wa Ligi ya Mabingwa Barani Africa CAFCL April 5, 2024

Michezo michezo miwili ya Ligi Ya Mabingwa Barani Afrika CAFCL ulipigwa usiku wa Ijumaa kati ya miamba wa Miisri Al Ahly dhidi ya Simba...

KIMENUKA BRUNO GOMES ATIMUKA SINGIDA FOUNTAIN GATE SABABU ZOTE ZAELEZWA

Bruno Gomes Atimuka Singida Fountain Gate. Kiungo mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Mbrazili Bruno Gomes ametangaza kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande...
SportsBENCHIKHA:- KWA CHAMA HUYU BADO HAMJASEMA NA MTASEMA

BENCHIKHA:- KWA CHAMA HUYU BADO HAMJASEMA NA MTASEMA

BENCHIKHA:- KWA CHAMA HUYU BADO HAMJASEMA NA MTASEMA. Miezi michache iliyopita Clatous Chama alikalia kuti kavu katika kikosi cha Simba, kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu uliomfanya asimamishwe kwa muda usiojulikana kabla ya kwenda fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zilizofanyika Ivory Coast akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Zambia.

Hata hivyo, kiungo mshambuliaji huyo alimalizana na mabosi wa klabu hiyo akiwamo Kocha Abdelhak Benchikha na kupiga kazi kwelikweli, kiasi cha kuzima hata zile kelele za mashabiki wa klabu hiyo waliotaka atemwe kabisa kikosoni.

BENCHIKHA:- KWA CHAMA HUYU BADO HAMJASEMA NA MTASEMA

Katika kuonyesha Chama ni kama amezaliwa upya, nyota huyo juzi usiku alioupiga mwingi kiasi cha kumfanya kocha Benchikha ashindwe kujizuia na kumwagia sifa kwa kiwango alichokionyesha kilichoisaidia Simba kuungan a na Yanga kwenye robo fainali na kuandika historia mpya Afrika ya Tanzania kuingia timu mbili kwa mpigo Ligi ya Mabingwa.

Chama alitembeza boli la kiwango cha juu wakati Simba ikiifyatua Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa mabao 6-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi B na kumaliza nafsi ya pili ikiwa na pointi tisa, mbili pungufu na ilizovuna vinara wa kundi hilo Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Katika mchezo huo, Chama aliwavuruga wageni akiifanya Simba iwe hatari eneo la mwisho la ushambuliaji akiwa ndiye aliyeingia mara nyingi zaidi katika eneo la penalti la Jwaneng Galaxy, akifanya hivyo mara mane kuliko mchezaji yeyote ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.

“Chama ni mchezaji hatari zaidi katika kukabiliana na mtu kwa mtu (one against one), na alichofanya leo (juzi) ni maajabu na kile ambacho mnakiona kutoka kwake ni kidogo katika uwezo mkubwa alionao. Ninyi bado hamjamuona Chama mwenyewe…,” alisema Benchikha.

RELATED